Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa 
sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la 
Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe.
Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa 
na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando 
kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu.
Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti 
hili lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu 
ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa 
msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo.
“Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa 
lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji 
wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia 
ishu zake,” alisema Nando.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”
 

