Furaha akiwa na marafiki zake akiwemo Kelly aliyesimama nyuma, mwimbaji wa Ambassadors.
Mmoja kati ya waimbaji wa muda mrefu wa
kundi la Ambassadors of Christ a.k.a Kwetu Pazuri aitwaye Furaha
Sandrine , jumapili iliyopita aliutambulisha rasmi ubavu wake uitwao
Ngabo Karangwa Tony katika sherehe ya kulipiwa mahari na kuvishwa pete
ya uchumba rasmi iliyofanyika nyumbani kwao maeneo ya Gikondo jijini
Kigali, ambapo harusi inatarajiwa kufanyika tarehe 6/7/2014 katika
kanisa la Wasabato la Gisenyi na kufuatiwa na shere ya kuwapongeza
itakayofanyika katika pwani ya Lac Kivu beach.
|