HII
ni kali lakini haikuwahi kuandikwa, staa wa Bongo Fleva, Ally Timbulo
alinusurika kuuawa baada ya kubainika kuwa anatembea na mke wa mtu na
mumewe kumsaka kwa udi na uvumba akiwa na bastola mkononi.
Akitema
cheche na Untold, Timbulo alisema, katika maisha yake hakuwahi
kufikiria kutoka kimapenzi na mtu ambaye yupo kwenye ndoa, isipokuwa
mwanadada huyo ambaye anafanya kazi serikalini (jina kapuni) alionesha
upendo wa dhati kwake pamoja na kumgharamia kwa kila alichohitaji.