Upelelezi
wa kesi ya kula njama ya kudhuru kwa sumu inayomkabili Mkurugenzi wa
Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Rwakatare na mwenzake Ludovick
Joseph, haujakamilika.
Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka alidai hayo jana mbele ya Hakimu
Aloyce Katemana wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo
ilipotajwa.
Hakimu
Katemana alisema kesi hiyo itatajwa tena Julai 8 mwaka huu kwa ajili ya
kuangalia kama upelelezi umekamilika. Washitakiwa wataendelea kuwa nje
kwa dhamana.
Hivi
karibuni Rwakatare kupitia kwa Wakili wake Peter Kibatala aliomba
upande wa jamhuri kumpa simu zake zilizochukuliwa alipokamatwa kwa ajili
ya kukamilisha upelelezi, hata hivyo upande wa Jamhuri ulidai
utawasiliana na polisi apewe simu hizo.
Rwakatare na mwenzake, Joseph wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama ya kudhuru kwa sumu.
Wanadaiwa
Desemba 28, mwaka juzi katika eneo la King’ongo wilayani Kinondoni,
walikula njama ya kutumia sumu kumdhuru Dennis Msacky wakati huo akiwa
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi.