Duru zinasema kuwa alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana wenye itikadi kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha yake.
Wengine waliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab huku wafuasi wao wakiilaumu serikali kwa mauaji yao, madai ambayo serikali imakanusha.
Marahemu Idris alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.