VIDEO: WATU WASIOJULIKANA WAMEIBA SANDUKU LENYE CHATU NA KULITELEKEZA JIJINI DAR


Watu wasiojulikana wameiba sanduku lenye chatu na kulitelekeza.
 Wakazi wa sinza uzuri jijini Dar es salaam wamepigwa na butwaa baada ya kuona nyoka aina ya chatu anayedaiwa kutupwa katika daraja,baada ya kusemekana kuwa kuna watu walioiba sanduku wakidhani lina fedha ndani yake na walipofungua wakakutana na joka aina ya chatu ndani yake na kutelekeza sanduku hilo na kukimbia kusiko julikana.
Manispaa ya Kinondoni imekemea uharifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya watu wanavunja sheria kwa kufanya biashara ovyo katika maeneo yasiyo rasmi na kwamba ili kukomesha tabia hiyo kuendelea wamepanga kuanza msako katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.
Katika kudhihirisha ushabiki wa damu wa michuano wa kombe la dunia linaloendelea nchini brazili,mashabiki fulani wamelazimika kupeperusha bendera ya marekani na uingereza katika nyumba zao maeneo ya kogogo post hali ilivutia watu wanaopita katika maeneo hayo kuuliza kulikoni.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...