WEMA SEPETU AWAJIBU WALIOMCHAFUA MAMA YAKE

Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu.

Sakata lenyewe lilianza hivi:
Baada ya picha feki ya Mama Wema kuwekwa mtandaoni na instagram account ijulikanayo kama Homa_ya_jiji_Team_Dengue na Account nyingine maarufu ya kumtetea Wema Ijulikanayo kama Dogiemasta13 ilifanya kazi ya ziada kumshawishi Homa_ya_jiji_Team_Dengue kuifuta hiyo picha na baada ya muda ilifutwa kwa masharti kuwa Dougiemasta13 aifunge account yake, na account ikafungwa kweli.
 
Wema ameandika hivu kwenye Instagram yake: Dah…! Sijui hata niseme nini…! Ila si mlitaka kuniumiza… leo mmefanikiwa… nawapeni hongera…. Tena mmetisha haswa… Kila sjku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu… Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo… I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it… Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo… Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu… mnataka afe na yeye nibaki yatima sio… dah… leo mmeniweza… saana jamani… Basi naomba isifike huko… nina uchungu sana na mama angu … nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu… Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako… una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama… dah… nime surrender leo…. hongera zenu narudia tena… mmeniweza leo…. dah… Mungu nipe nguvu ktk hili jamani… Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba…. Eeeh mungu… Dah… Ila nashkuru….


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...