Mwanafunzi
wa darasa la sita anayesoma shule ya msingi (jina linahifadhiwa
kimaadili) amekutwa kwenye kambi ya machangudoa akidaiwa kujihusisha na
biashara haramu ya kuuza mwili.Tukio
hilo lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Kahumba mjini Morogoro usiku wa
manane ambapo chanzo kilipokea simu kutoka kwa watu walioumizwa na jambo
hilo huku wakimwonea huruma kwani alikuwa akichukuliwa na mijibaba.
Chanzo
kilipofika eneo la tukio kilimshuhudia binti huyo lakini ilipotaka
kuita polisi, wenzake waliokuwa wakijiuza naye walikuja juu wakitaka
kumshushia kipigo mwanahabari wetu.
Kesho
yake Chanzo kilikwenda kumsaka mtoto huyo ambapo mama aliyejitambulisha
kwa jina la Nasra Hamis Ndehere alikuwa miongoni mwa wazazi
waliojitokeza baada ya kukerwa na tabia ya mtoto huyo ya kujiuza.
Baada
ya kumnasa, binti huyo alikiri kujihusisha na biashara hiyo haramu kwa
kisingizio cha ukali wa maisha baada ya kufiwa na wazazi wake, alidai
alikuwa akitafuta pesa ya kununulia nguo za Sikukuu ya Idd.
Pia
mtoto huyo alidai kuwa nyumbani kwao ni Mwanza na alipoulizwa kama
anaweza kuwasiliana na ndugu zake alijibu anaweza hivyo alipewa simu ili
awapigie lakini namba zao hazikuwa hewani.
Baada ya kuona hali hiyo, chanzo kwa kushirikiana na mama huyo waliamua kumpeleka mtoto huyo Ustawi wa Jamii.
Katika
hali ya kushangaza, wakati wanaelekea Ustawi wa Jamii, walikutana na
msichana ambaye baada ya kuwaona alisema binti huyo siku hizi haonekani
shuleni kwani anasoma naye darasa moja.
Kufuatia kauli hiyo, mama huyo alimshushia kichapo kikali denti huyo hivyo kujaza umati.
Baada
ya kuona hali hiyo, chanzo kilijitosa kumnusuru denti huyo kwa kuita
polisi wa pikipiki ambao walifika fasta na kumpeleka mtoto huyo kituo
kidogo cha polisi Kata ya Mji Mpya mjini hapa ambapo alikabidhiwa kwenye
Dawati la Jinsia.