JB: SITAKI KUGEUZWA DARAJA

Stori: Jelard Lucas
MKONGWE kwenye sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ amewakemea chipukizi ambao wanatamaa ya kutoka kupitia jina lake na kuwaambia yeye siyo daraja.

 
Jacob Steven ‘JB’.
Akizungumza na paparazi wetu, JB alisema yuko tayari kuendeleza kipaji cha msanii ambaye tayari ameshaanza sanaa akiwa na kipaji cha kweli na hana tamaa ya umaarufu na si wimbi kubwa la wasanii ambao wana uchu wa kusaka umaarufu kupitia sanaa.
“Hata watu wanichukie mimi sijali kwani kipaji cha kweli kinaonekana dhahiri na huwa sipendi kumpa mtu umaarufu wakati hana kipaji, kimsingi nipo kwa ajili ya kuendeleza kipaji, sitaki kuwabebabeba chipukizi ili watoke kupitia jina langu,” alisema JB na kuongeza:
“Unaweza kubebwa leo kwa lengo la kuonekana katika runinga kwa kipindi kifupi lakini baada ya muda unapotea, sasa hapo itakuwa na maana gani si bora nisiwasaidie kabisa kuliko kuwabeba wasiobebeka.”


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...