Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa majeshi ya Kenya yataendelea kukaa Somalia hadi usalama utakapoimarishwa katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya miaka mingi. |
Rais Kenyatta amesema kuwa nchi yake haitashurutishwa na magaidi walioteka jengo la maduka la Westgate kwa siku 4.
Rais
Kenyatta alihutubia umati uliokusanyika kwa maombi ya pamoja ya dini
mbali mbali, kwa ajili ya watu 67 waliouawa katika shambulio la
Westgate.
Shambulio hilo ndio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Kneya tangu majeshi yake yaingie nchini Somalia mwaka wa 2011.
''Hawa
wauaji waliokuja kutenda ukatili wao ulio na woga hapa nchini kwetu,
walikuwa wanadai kuwa wanafanya hivyo kwasababu majeshi ya Kenya yapo
nchini Somalia. Nataka niwaeleze bayana kuwa, majeshi yetu yatakaa huko
hadi kuwepo amani katika nchi hiyo.''
Mmoja
wa makasisi walioongoza maombi hayo, alisema,'' Baba tunakuomba utawale
nchi hii. Na uwaoneshe maadui wote wa taifa hili kuwa wewe unaipenda
nchi hii na jina lako litatukuzwa.''
Wapiganaji
hao wa Al Shabaab wamesema kuwa walifanya shambulio hilo kulipiza
kisasi kwa namna majeshi ya Kenya yaliingia na kuwapiga nchini Simalia.