KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAENDESHA UKAGUZI WA MAGARI KWA WAFANYAKAZI WA AIRTEL‏

CPL Jumaa Mwalimu wa kituo cha polisi Oyesterbay akikagua gari la mmoja wa wafanyakazi wa Airtel  Bi. Susan Kajubili wakati  polisi kikosi cha usalama barabarani kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi wa Airtel katika kutimiza lengo la wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Zoezi hilo lilifanyika katika makao makuu ya Airtel Morocco.
CPL Jumaa Mwalimu wa kituo cha polisi Oyesterbay akikagua tairi la gari la mmoja wa wafanyakazi wa Airtel  James Majwala wakati  polisi kikosi cha usalama barabarani kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi wa Airtel katika makao makuu ya Airtel Morocco.
Mfanyakazi wa Airtel bwana Jacob Malisa akibandika stika ya usalama barabarani mara baada ya gari lake kukaguliwa na kuthibitishwa kufaa kutembea barabarani. Zoezi la ukaguzi wa magari lilifanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuwashirikisha wafanyakazi wa kampuni hiyo.
CPL Jumaa Mwalimu wa kituo cha polisi Oyesterbay akikagua uhalali wa stika ya leseni ya barabarani katika moja ya gari la mfanyakazi wa Airtel Bwana Francis Ndikumwami wakati  polisi kikosi cha usalama barabarani kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi wa Airtel  katika makao makuu ya Airtel Morocco.
Inspekta Serengeti Action wa kituo cha polisi Oyesterbay akiingia katika moja ya gari la mfanyakazi wa Airtel Bi. Aminata Nakieta tayari kwa ukaguzi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...