KIZIMBANI KWA KUKOJOLEA QURAN TUKUFU‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi

Mtu mmoja Mkazi wa Nsemulwa Kichangani  mjini Mpanda  Mkoa wa Katavi Jafeti  Nobeti (15)  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  mfawidhi mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Chiganga Ntengwe kwa tuhuma za kukojolea Quran Tukufu

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo hapo juzi majira ya saa tano asubuhi katika eneo la msikiti wa Kichangani uliopo  katika mtaa wa Nsemlwa mjini hapa

Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi  Mwandolomi aliileza Mahakama kuwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alikojolea Quran  hiyo ambayo ilikuwa imewekwa na watoto wa kisramu  ambao walikuwa wakisoma madrasa iliyoko katika msikiti huo

Ilielezwa wakati watoto wa madrasa wakiendelea  na mchezo wa mpira wa miguu wakati wa kipindi cha mapumziko  ndipo mtuhumiwa Jafeti alipofika kwenye eneo hilo akitokea kwao  ambapo ni jirani na msikiti huo

Watoto wa Madrasa wakati wakiendelea na mchezo wa mpira ndipo walipo mwona mtuhumiwa akiwa anakojolea Quran  hiyo hari ambayo iliwashitua na kumfuata mtuhumiwa na kuanza kumshambulia kwa kipigo

Mtuhumiwa aliendelea kupokea kipigo hadi hapo alipokuja kuokolewa na mwalimu wa Madrasa hiyo Ustadh Khalfan Juma na Shekhe wa mtaa Shekhe Yusuph Mkumba ambao walilazimika kumuhifadhi kwenye nyumba ya mwalimu wa madrasa hiyo na baada ya hali kuwa tulivu walimpeleka kwenye nyumba ya mwalimu huyo na kisha hali ilipokuwa shari walimpeleka kwenye kituo cha polisi cha mpanda mjini

mtuhumiwa baada ya kusomewa mashtaka alikiri kutenda kosa hilo lakini alieleza kuwa hakufanya kitendo hicho kwa maksudi bali wakati alipokua akikojolea hakujua kama ni Quran alidhani kuwa ni kasha la kuhifadhia kanda za video

hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mtuhumiwa kusomewa mashtaka na kukiri kutenda kosa hilo bila kukusudia aliahirisha kesi hiyo hadi hapo Nov 14

hata hivyo mtuhumiwa aliweza kupata dhamana baada ya kutimiza masharti ambapo alitakiw adhaminiwe na mtu mmoja kwa dhamana ya shilingi milioni moja na nusu kwani hakimu Chiganga kutokana na umri wa mtuhumiwa kuwa mdogo isingekuwa busara kwa mtuhumiwa kupelekwa mahabusu
 
Via
http://kataviyetu.blogspot.com


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...