Ikiwa
ni mwezi mmoja na siku kadhaa zimepita tangu kutokea kwa tukio la
kigaidi la uvamizi wa maduka ya Westgate mjini Nairobi yaliyofanywa na
kundi la wanamgambo
wa al-Shabaab, asubuhi ya leo ya Novemba 7 2013, mamlaka za usalama
Mkoani Mwanza zimefanya uvamizi kwenye hoteli ya Gold Crest ya jijini
Mwanza.
Uvamizi
huo ambao kwa taarifa za awali kutoka katika vyanzo vyetu lilikuwa ni
la jaribio kuona uwezo na namna ya wananchi na jamii kwa ujumla
wanavyoweza kukabiliana na matukio ya aina hiyo.
Hata
hivyo tukio hilo lililochukua muda wa saa nzima limeibua takaruki kwa
wananchi waliokuwa ndani ya hoteli na nje ya hoteli hiyo jambo
lililopelekea umati wa watu wengi kukusanyika kwa lengo la kujua nini
kinachoendelea.
Hakika
kwa utamaduni huu wa watanzania kukimbilia kwenye eneo la tukio badala
ya kukimbia sehemu salama kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kama
tukio kama hili likitokea katika mazingira ya uhalisia (tunaomba manani
atuepushe na mabalaa ya namna hii). Tazama picha zote za tukio hili
lakini nitoe angaliazo tu kuwa TUKIO HILI NI LA MAJARIBIO NA LIMEFANYWA KWA KUSHTUKIZA.