Wafanya biashara wa Mkoa wa Morogoro wakiwa wamekusanyika wakijadili jambo.
Wafanyabiashara
wa Mkoa wa Morogoro wamegoma kufungua maduka leo wakitaka kuonana na
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za
kieletroniki za mamlaka ya mapato tanzania.Wafanya biashara hao wamegoma
kufungua maduka
tangu asubuhi wakishinikiza kuonana na mkuu wa mkoa jambo ambalo Mkuu
wa mkoa amekubali na kuwaomba wateuliwe wawakilishi 8 kwa ajili ya
kwenda kuonana naoa.Baada ya wawakilishi kuteuliwa bado wafanyabiashara
hao walishinikiza kuandamana mpaka nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndipo
Jeshi la Polisi walipoingila kati .
Jeshi la
Polisi wakiwa barabara inayoelekea Kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Kulinda Amani na kuzuia maandamano yaliofanywa na
wafanyabiashara hao muda huu.
Waduka yakiwa yamefungwa katikati ya Mji wa Morogoro
Wafanyabishara
hao wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo
la kushinikiza kuondolewa kwa mashine za Kieletroniki kwa madai kwamba
ni kikwazo kikubwa katika biashara zao za kila siku
Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi