Mwakilishi
wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto, Bw. Emmanuel Mzava,
akionyesha waandishi wa habari vifaa vya michezo vilivyotolewa na Bw.
Davis Mosha. Kulia ni Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK
Media Group Bw. Alex Kassuwi.
Na Ngonise Kahise
Kampuni ya Delina Group (DGE) inayomilikiwa na Bw. Davis Mosha imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya mamilioni ya pesa pamoja na vikombe kwa ajili ya kumtafuta Bingwa wa Uhuru Cup kwa timu za mpira ambazo zinaundwa na watanzania ambao wanaishi nchini Marekani na ni mashabiki wa Simba na Yanga. Tarehe za mechi hizo zitatajwa hivi karibuni tukishirikiana na ubalozi wa Tanzania.
Kampuni ya Delina Group (DGE) inayomilikiwa na Bw. Davis Mosha imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya mamilioni ya pesa pamoja na vikombe kwa ajili ya kumtafuta Bingwa wa Uhuru Cup kwa timu za mpira ambazo zinaundwa na watanzania ambao wanaishi nchini Marekani na ni mashabiki wa Simba na Yanga. Tarehe za mechi hizo zitatajwa hivi karibuni tukishirikiana na ubalozi wa Tanzania.
Mwakilishi
wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto, Bw. Emmanuel Mzava,
akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa mashabiki wa Simba na Yanga
wanaoishi Marekani Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media
Group Bw. Alex Kassuwi (kulia).
Aidha Emmanuel ameongeza kuwa,lengo la Kampuni ya Delina Group
(DGE) kudhamini timu hizo zinazoundwa na mashabiki wa Simba na Yanga
zilizopo ugenini,ni kuweka hamasa ya ushindani ndani na nje ya nchi na
kuongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu.
Kutoka kushoto ni Emmanuel Mzava wa Delina Group (DGE) na kulia anayezungumza ni Alex
Kassuwi Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group
wamiliki wa Swahili Radio Online, Swahili TV online, Swahilitv blog, na
DMK411 blog.
Kwa habari zaidi tembelea
www.swahilitv.blogspot.com