Stori: Issa Mnally
KRISMASI noma sana! Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Pendo
ameiona chungu Sikukuu ya Krismasi 2013 kufuatia tukio la kufumaniwa na
mkewe, Mama Pendo au Mama P ‘akibanjuka’ na mwanamke ndani ya gari.
NI MKESHA WA KRISMASI
Tukio hilo la aina yake
lilijiri eneo maarufu Kijitonyama jijini Dar linalojulikana kwa jina la
Miti Mirefu, usiku wa Mkesha wa Krismasi, majira ya saa 8:00 usiku wa
kuamkia Jumatano iliyopita.
Ina maana kwamba Baba Pendo aliamua ‘kumalizia shida’ zake ndani ya gari hilo ambalo namba zake za usajili tunaziweka kapuni.
OFM YAJUZWA
Kabla ya tukio hilo, mara kadhaa
Mama P aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global
Publishers na kulalamika juu ya mumewe kutoka nje ya ndoa na mwanamke
mmoja wa mjini.
Mama P: Haloo…naongea na OFM? Jamani naombeni mnisaidie kuna mwanamke anamzuzua sana mke wangu.
OFM: Una uhakika mama?
Mama P: Nina uhakika wa asilimia mia moja. Hapa nimeona meseji
wamepanga kukutana leo na ndiyo maana nikawatafuta. Ninyi mpo wapi?
OFM: Sawa, sisi tupo kikazi Mango Garden (Kinondoni, Dar) wewe upo wapi?
Mama P: Nipo Sinza A (Dar) nitawashtua mambo yakiiva maana najua lazima mume wangu atatoka muda si mrefu, nimemuona anajiandaa.
OFM: Oke lakini uwe makini sana.
Mama P: Sawa, nitawashtua.
Hiyo ilikuwa saa 5:12 usiku, hivyo OFM iliendelea na majukumu mengine ya kufichua uovu katika jamii.
BABA PENDO AAGA ANAKWENDA MKESHA
Kwa mujibu wa
Mama P, majira ya saa 5:20 usiku, mumewe alimuaga anakwenda kwenye
mkesha wa kumpokea mwana wa Mungu (Yesu) aliyezaliwa ambapo kwa mujibu
wa mume huyo, alikuwa anakwenda kusali Kanisa la Mtakatifu Maximilian
Kolbe lililopo Mwenge, Dar.
MAMA P MZIGONI
Baada ya mumewe kuondoka,
mwanamke huyo aliwasiliana na OFM na kuwapa ishu nzima ambapo walimpa
mbinu ya kumfuatilia mumewe ikiwa ni pamoja na kubadili aina ya usafiri
ili asishtuke.
Mama P alichukua Bajaj na kumfuatilia mumewe hadi maeneo ya
Sinza-Kijiweni ambapo alimuona akipaki gari lake na kuingia kwenye
‘pabu’ moja kisha akaagiza ‘ngumu kumeza’ (mzinga wa konya) ambayo
aliipiga taratibu hadi mishale ya saa 8: 05 usiku huku akipiga stori na
washkaji.
Baada ya hapo, Baba Pendo aliingia garini kuondoka. Mama P naye akachukua bodaboda kumfuatilia kwa nyuma.
Alipofika maeneo ya Kijitonyama alimuona akisimamisha gari na kuingia
kwenye ‘kamtaa’ f’lani, akatoka na mwanamke kisha akaingia naye kwenye
gari.
Alisema yeye akiwa bado nyuma, walipofika Miti Mirefu mumewe alipaki gari lakini hakuna aliyeshuka.
Aliendelea kusimulia kisa mkasa mbele ya ‘kachero’ wa OFM kuwa
uvumilivu ulimshinda, alihisi kuna linaloendelea ndani ya gari, akaamua
kulisogelea na ndipo hamadi! Akamkuta mumewe ‘laivu akiduu’ na mwanamke
huyo na ndipo OFM walipochomoza baada ya kujulishwa kuwa ishu imetiki.
“Uzuri ni kwamba walisahau ‘kuloki’ milango ya gari ‘so’ nilipoushika
ukafunguka,” alisema Mama P baada ya OFM kupiga picha za kutosha.
TIMBWILI
Katika tukio hilo kulitokea timbwili
ambapo askari waliokuwa doria walitonywa na kufika eneo la tukio na
kuamulia damu isimwagike.
Mwanamke aliyenaswa na mume wa mtu alikula mbata za kufa mtu huku mwanaume akitoka nduki kukwepa aibu ya kamera za OFM.
MAMA P HASIRA
OFM ilimsikia Mama P akisema:
“Kumbe ndiyo wewe…nilikuwa nakufuatilia muda mrefu, badala ya kwenda
kanisani unahangaika na waume za watu hata humuogopi Mungu.”
Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, wanawake hao walikuwa
mikononi mwa polisi wakitakiwa kuacha ugomvi na kama kuna malalamiko
wayafikishe kituoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)