Mshindi
wa Shindano la Maisha Plus Bernick Kimiro akizungumza na wageni wa
alikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa
kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano
la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimesha anza
kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za
kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.
Mtaalam
wa Mambo ya Mbogamboga na Mshauri katika maswala ya kilimo kutoka OXFAM
Bwana Zephaniah akizungumzia kuhusiana na uzinduzi wa Maisha Plus/Mama
shujaa wa Chakula 2013 , na kueleza faida za kilimo na kuwekeza kwa
wakulima wodogo wadogo.
Dr. Emmanuel Tumusiime kutoka OXFAM akifanya uzinduzi rasmi wa Ripoti
ya 'Feed the Future Initiative in Tanzania' ambapo katika ripoti hiyo
kuna mambo ya msingi ya kulinda chakula kisije kikaja kuisha na Taifa
likaja kukosa kabisa siku za mbeleni.
Bwana Bonda ambaye ni mmoja wa wakurugenzi Maisha Plus.

Kulia ni aliyekuwa Mshindi Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sr. Matha Mwasu akiwa na Mshindi wa Tatu Bi. Tatu
Kutoka Kulia ni Mshindi wa Pili wa wa Maisha Plus Venance Mushi akiwa
na Mama shujaa wa chakula wa kwanza wa mwaka 2011 Bi. Ester Mtegule
pamoja na Aliyekuwa mshiriki wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula 2011
Bi. Dora Myinga

Mdau kutoka OXFAM Bill Marwa Akiwa anafuatilia kwa umakini uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula 2013 Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akifanya uzinduzi wa aina yake
wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012/13 kwa kufukua fomu ambazo
zilikuwa zimefukiwa ikiwa ni kielelezo cha kilimo kwanza
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. AnthonyMtaka akizionesha fomu hizo baada ya uzinduzi huo.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akimkabidhi Fomu ya
kwanza ya ushiriki kwa Bi. Nuru Saidi Mbonga kutoka Dakawa ikiwa ni fomu
ya Mama shujaa wa Chakula 2013
Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya
Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani.
Mmoja ya Vijana wakiume nae akiwa anakabidhiwa fomu ya ushiriki na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka.

Wakiwa wanasoma fomu na kujiandaa kuzijaza.
Waliovaa T-Shirt za Rangi nyeusi ni Wadau wa OXFAM.

Burudani za Ngoma zikiendelea.

Burudani za aina yake zikiendelea.

Wazee kutoka eneo la Kingolwira wakiwa wamekuja kushuhudia uzinduzi huo.

Wadau kutoka Sehemu mbalimbali wakiwa wamekuja shuhudia uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Ali Masoud 'Kipanya' akifunga sherehe fupi za uzinduzi wa Maisha Plus 2013