STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi ameingia kwenye majanga baada
ya kudaiwa kukacha na deni la prodyuza Mohammed Kandoro wa Studio za
Fire Music ambaye alimrekodia nyimbo kadhaa wakati akisaka kutoka...
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Snura ameingia
mitini na kiasi cha Tsh. 400,000 za prodyuza huyo na kwamba sasa
amehamia studio nyingine.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Kandoro na kumwuliza kuhusu
ukweli wa minong’ono hiyo, ambapo alikiri na kusema: “Ni kweli namdai
laki nne. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu lakini sasa naona ameamua
kuondoka na deni langu.”
Snura alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu madai hayo, alifunguka:
“Kama kuna deni basi meneja wangu HK (Hyper Man) ndiye anayehusika,
maana kila kitu nilimkabidhi yeye na naamini alilipa, sasa kama hakulipa
hayo ni mambo yanayomhusu yeye, si mimi tena.”
Katika kutafuta mzani wa habari, gazeti hili liliwasiliana na meneja
wa Snura, HK ambaye alisema hana deni lolote analodaiwa na Kandoro,
ingawa alikiri kumhamisha Snura studio.
“Kilichopo ni kwamba tumehama kwenye hiyo studio, sina ugomvi nao
wala Snura hajawahi kutofautiana naye. Tumefanya hivi kwa lengo la
kutafuta ladha tofauti... hayo mambo ya madeni, si kweli.
Hivi kama leo hii tunaweza kulipa zaidi ya shilingi milioni moja na
laki nne (1,400,000) tunashindwaje kulipa laki nne tu? Hayo ni maajabu,”
alisema HK.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)