BAADA
Mei mwaka huu kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la
kufanya ukahaba, mkazi wa jijini Dar, Blandina Barton amekamatwa tena
kwa kosa hilohilo ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kumaliza kifungo
chake,..
Habari
za uhakika zilizopatikana katika Mahakama ya Jiji, Dar es Salaam
zinasema kwamba mfungwa huyo alitumikia kifungo chake katika Gereza la
Segerea jijini Dar na alipobakiza miezi michache kumaliza alionewa
huruma na bibi jela na kutakiwa kumalizia kifungo hicho uraiani.
Inadaiwa kuwa kabla ya kuachiwa, bibi jela alimsihi Blandina kuhakikisha harudii kosa lililompeleka gerezani pindi atakapokuwa akimalizia kifungo chake nje ya gereza.
Blandina akamhakikishia bibi huyo kwamba atakuwa mtu safi kwani amejifunza vya kutosha.
Katika hali ya kushangaza, Jumatano iliyopita Blandina alipandishwa tena katika Mahakama ya Jiji iliyopo Barabara ya Sokoine jijini Dar akiwa amerudia kosa lililompeleka Segerea miezi michache iliyopita.
Imeelezwa
mahakamani hapo kwamba, Septemba 24, mwaka huu Blandina na wenzake
wanne walinaswa Buguruni usiku wakiwa katika mawindo ya ukahaba.
Bahati
mbaya kwa Blandina alipofikishwa mahakamani hapo alikutana na hakimu
yuleyule aliyemhukumu kifungo cha miezi sita kwa kosa la ukahaba.
Sharti
hilo lilionekana kuwa gumu kwa watuhumiwa wote, hivyo walipandishwa
karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Oktoba 15, mwaka huu
kesi yao itakapotajwa tena mahakamani hapo....
Hakimu huyo, Timothy Lyon alipigwa na butwaa baada ya kumuona Blandina akiwa amesimama mbele yake.
Mtuhumiwa
huyo aliyekuwa na wenzake, Husna Amos, Monica Denis, Esther Chizai na
Angela Emmanuel wote kwa pamoja walisomewa mashtaka yao na kukana.
Hakimu
Lyon aliwaambia watuhumiwa hao kwamba dhamana iko wazi na kuwataka kila
mmoja kuwa na wadhamini wawili na shilingi laki mbili