Juma Mwambelo.
Na John Joseph ALIYEJITANGAZA
kuwa mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari
kukabidhi nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano
wa Yanga kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga
kimakosa na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya
kuchukuliwa hatua.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari
kumpa Rais Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga,
ila Rais Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani
nimewahi kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.
“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya
klabu, hii hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia
ninayo ya jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti
polisi.
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.
“Nashangaa Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali,
katiba halali ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa
(anaonyesha),” alisema.
Alipoulizwa juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo,
alisema: “Wanachama wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko
mwaka 1975, wanachama halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna
wanachama halali tena, hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.
“Hapa nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya
kujihami, nahofia kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,”
alisema.
Katika mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume,
PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma
kuwa ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.
“Mimi nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano,
tangu pale sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata
huyo Mrisho Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa
ninachotaka ni utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza
huku akitabasamu.