Nasibu Abdul Almaarufu kama Diamond
Plutnum ni kati ya wasanii hapa nchini ambao wamekuwa wakionyesha upendo
wao wa dhati kwa mama yake mzazi kiasi cha kuamua kuwa naye katika
maeneo mengi hata anapopata nafasi ya kupiga show ndani na nje ya
nchi kitu ambacho kimeonekana kukera baadhi ya mashabiki zake na
kuhoji kuhusiana na hilo .
Alisikika mdau mmoja ambaye ni shabiki mkubwa sana wa msanii huyo diamond plutnum akihoji juu ya hali hiyo nakuonekana kukereka .
“unajua wasanii wengi sana wana mama zao na kila mmoja anampenda sana mama yake mzazi kwa namna moja ama nyingine lakini kwa upande wangu mimi nahisi kama nakwazika kwa hili la Diamond , maana kila mahali anaenda na mama yake hata katika shows anazoenda kupiga za usiku yupo na mama yake, sasa ndo kumpenda sana au ???” alihoji shabiki huyo

mbali na huyo yupo pia mwingine
aliyejitambulisha kwa jina la Subira Chacha wakati akizungumza na
blog hii , ambaye yupo katika manispaa ya musoma naye alisema kitu
kinachoboa zaidi ni tabia ya msanii huyo kuambatana na mama yake mzazi
kila mahali.
“Diamond Plutnum ni msanii mzuri sana
maana mi mwenyewe ni shabiki wake ila ananiboa kitu kimoja tu ,tabia ya
kuambatana na mama yake mzazi kila mahali, duh, inaniboa kiukweli hata
kama ni upendo huo wake umepitiliza.”alisema
Naye Blogger Wa Blog Ya Jicho La
Mdadisi na ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo Cha Radio Victoria Fm
90.6 Kilichopo Musoma Mara ,Bwana Ahmad Nandonde katika hilo yeye
alisema haina tatizo isipokuwa sio utamaduni ambao umezoeleka sana kwa
hapa nyumbani ndio maana wengi wanaboreka.
“sijaona kama ni tatizo kwa msanii huyu
kuambatana na mama yake mzazi kila mahali ,lakini pia inabidi yeye
mwenyewe awe anaangalia kama ni sahihi kwa upande wake au la , na pia
unajua hili wengi linawaboa lakini ni kwaajili tu haijazoeleka kwa hapa
kwetu msanii kuambatana hivyo na mama yake mzazi kila mahali na hasa
katika shows zake.”alisema Ahmadi
Diamond Plutnum alipotafutwa kuhusianaa
na hili hakuweza kupatikana kwasababu ambazo zilielezwa kuwa ndio
alikuwa anarudi hapa nchini leo hii baada ya kupiga show yake huko
nchini Kenya .