KAMA
ulikuwa hufahamu, habari kuu katika ulimwengu wa Teknohama kwa siku ya
leo ni Facebook kuinunua Whatsapp kwa bei ya dola bilioni 19. Ununuzi
huo ni wa programu pekee na siyo kampuni ingawa wafanyakazi wa Whatsapp
watajiunga na timu ya Facebook moja kwa moja na kazi za Whatsapp
zitaendelea kubaki kama zilivyo, alieleza Jan Koum ambaye ni muanzilishi
wa Whatsapp.
Kwa wasiofahamu, Whatsapp ni moja ya programu za simu za mkononi
inayokuwezesha kutuma ujumbe wa simu kupitia kwenye Intaneti badala ya
ujumbe mfupi (sms). Kwa kutumia Whatsapp, ina maana utaepuka gharama za
sms huku ikiwa imesheheni matumizi mengine mengi zaidi kama kutuma
picha, sauti uliyojirekodi, nk.
Hadi sasa, Whatsapp ina watumiaji hai milioni 450 kila mwezi kutoka
nchi nyingi duniani, huku kukiwa na watumiaji wapya zaidi ya milioni
moja kila siku. Hivyo, ni dhahiri kuwa Whatsapp ni programu pendwa na
yenye kutumika.
Whatsapp inaweza kutumika kama njia rahisi zaidi ya mawasiliano kwa
watu binafsi na hata makampuni