Kijana mmoja
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 ameuawa kwa kupigwa mawe kisha
kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa na
pikipiki ya wizi Katika kijiji cha kagongwa Wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa nane Mchana mara baada ya marehemu
kuiba Pikipiki hiyo yenye no T634 CNK Aina ya SanLG mali ya Patrick Seba
mkazi wa Nyahanga Mjini Kahama ambayo imeibiwa jana Asubuhi Maeneo ya
shule ya Kahama Musilim ikiwa imeegeshwa na dereva wake aitwaye Shija
Zacharia.
Kwa
mujibu wa Mmiliki wa pikipiki hiyo Bwana Seba Ameiambia redio Kahama fm
Kuwa alipewa taarifa na dereva wake ambpo aliamua kutoa tarifa ya
upoteza pikipiki hiyo kwa waendesha bodaboda wa mjini Kahama na
Kagongwa.
Amesema wakati anatoka Kagongwa kutoa taarifa ndipo akakutana na
vijana wawili ambao walikuwa wanaiendesha pikipiki hiyo kuelekea
Kagongwa ambapo aliamua kuwafuatilia na kwamba aliwapata katika kijiji
hicho.
Baada ya
kuwasogelea aliizima pikipiki hiyo kwa kutumia remote kwani wakati
inaibiwa ilikuwa imezimwa kwa kutumia Remote ambapo walianguka china na
Kuanza kukimbia huku wananchi wakaanza kumshambulia mmoja kwa mawe hadi
kumuua huku mwingine akifanikiwa kukimbia kusikojulikana.
Hata
hivyo jeshio la Polisi wilayani Kahama limedhibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa kuhifadhiwa katika chumba
cha kuhifdadhia maiti kwenye hospitali ya Wilaya ya kahama.
Kwa takribani miezi Miwili na Nusu sasa watu wa wanne wameuawa kwa
kuchomwa na moto katika kijiji hicho kwa madai kuwa wamechoshwa na
kukithiri kwa wimbi la wizi katika Kijiji hicho na maeneo jirani.
chanzo: Dunia Kiganjani