Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhwan Kikwete akionesha fomu aliyochukua ya kugombea ubunge jimbo hilo. Kulia kwake ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo, Kongo Kamate na Mbunge wa viti maalum wa Jimbo la Chalinze, Subira Mgalu.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Ridhwan Kikwete akijaza fomu ya kugombea jimbo hilo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ridhwan Kikwete akiongozana na wanachama wa CCM kwenda kuchukua fomu
fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete jana alichukua fomu
katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi wilayani Bagamoyo na leo anatarajia kurudisha fomu hiyo.
Akisindikizwa na mamia ya wanachama na
mashabiki wa CCM wa Jimbo la Chalinze na Bagamoyo, Ridhwani
alimhakikishia ofisa wa uchaguzi wa wilaya ya Bagamoyo Shija Andrew,
kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na kutoendesha kampeni za matusi na vurugu.
Baada ya kuchukua fomu hiyo pamoja na nakala nyingine muhimu za
uchaguzi aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake kuelekea kwenye ofisi
za CCM Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa
habari. Katika
mazungumzo yake hayo Ridhwan alitaja vipaumbele vyake kwa kuleta
maendeleo kwa wakazi wa Chalinze ambapo alisisitizia kuimarisha
upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha
afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
"Kama mnavyofahamu kuwa
Chalinze ni eneo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi kama vile
maji, umeme na hata suala zima la ajira kwa vijana sasa pindi ambapo
nikipata Ubunge kwangu mimi nitahakikisha kuwa napunguza kama sio
kumaliza kabisa tatizo hilo" alisema Ridhwan.
Aliongeza kuwa "Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali
zinazowakuta wakazi wa wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa
sikushinikizwa ila ni kwa matakwa yangu mwenyewe naona kabisa kuwa nipo
katika hali na nguvu ya kushirikiana na wananchi kumaliza shida za
Chalinze".
Ridhwan pia alisema kuwa
atasaidia kutatua ugomvi wa mara kwa mara unaowakumba wakulima na
wafugaji na kuwataka wakazi wa Chalinze kumchagua kwa kishindo. Wakati huo huo mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey akizungumza baada ya kuchukua fomu
alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua maisha ya wakazi wa Chalinze.
Leo Ridhwan anatarajiwa kurejesha fomu za kugombea ubunge katika ofisi ndogo za uchaguzi.alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua maisha ya wakazi wa Chalinze.
Uchaguzi wa jimbo la Chalinze unakuja kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ramadhan Bwamdogo aliefariki Januari 22 mwaka huu