AJARIBU KUJIZIKA KUKWEPA MATATIZO YA NDOA KENYA

MWANAUME mmoja nchini Kenya amewaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la Ufa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift Valley.
Mwanaume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua, hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndio maana akaamua kujitoa uhai.
Mwanaume huyo kwa jina Kipsang, alichimba kaburi hilo usiku na kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanaume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanaume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya ndizi eneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.
Chanzo: BBCSWAHILI


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...