Ndugu
Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi, angalau kusaidia Lori hilo
pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili, wapite nae
msafara wake uweze kuendelea na safari.
Sehemu
korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao
uweze kupita, lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara
wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
Ndugu
Kinana akizungumza na baadhi ya Wanahabari aliokuwa ameambatana nao
kwenye msafara wake, baada ya magari kunasa kutokana tatizo la barabara.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu
Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini,
Mh. Ali Mohammed Kessy, walipokuwa wakitembea kwa miguu kufuatia msafara
huo kukumbana na changamoto ya barabara mapema jana jioni katikati ya
Msitu wa hifadhi ya wilaya ya Nkasi. Ndugu Kinana na Msafara wake
ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha Mwampemba
kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2010. Barabara
hiyo yenye urefu wa kilometa 100, lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12
kwenda na kurudi kutokana na ubovu wa barabara. Ndugu Kinana yuko Mkoani
Rukwa, Katavi na Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha
CCM, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero
mbalimbali za wananchi.
Wanahabari
waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana wakiwa hoi
kabisa, wakisubiri kudra za Mwenyezi Mungu, msafara wa magari yao
yanasuliwe na kuendelea na safari. Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu,
Ndugu Kinana.
Hali ilikuwa tete mnoo, kipande cha kilometa mia kinapitika kwa zaidi ya masaa sita, kutoka kijiji kimoja kwenda kingine.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana (alinaerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa mawe, ili msafara uweze kupita.
Pichani
kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi
ya barabara kwa miguu, huku madera wakipiga hesabu zao namna ya kupita.
Mchuma ukipita sehemu korofi ya barabara kwa mbinde.
(PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA)