Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu
Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea
usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma katika bandari ya Karema
mkoani Katavi, ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia
mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne. Kinana pia
alipata nafasi ya kupita ufukweni mwa ziwa Tanganyika na kukutana na
baadhi ya wavijiji kuwasilikiliza matatizo yao.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaaf Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku
huu kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana na Viongozi wengine wa Taifa, Mkoa na Wilaya
tayari kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake
(hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea
mkoani Kigoma katika bandari ya Karema mkoani Katavi, ambako amemaliza
ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na
ziara ya siku nne.
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa
Karema mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani
Kigoma kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa
masaa kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya
majini,inaelezwa kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu
huyo, Kinana umepotewa ziwa la Tanganyika, jambo amabalo si la kweli na
la kizushi.
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na
Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye
bandari ya Karema mkoani humo usiku huu. Kinana ameongoza na Katibu Wa
NEC,Siasa na Uenezi, Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume, Mkuu
wa mkoa wa Kigoma, Kanal Issa Machibya, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa
Kigoma ndugu Kabouru na wengineo.
Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.
(PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-KATAVI)