MH.MGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI JIMBONI KWAKE

 Mbunge wa  jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura wake katika kijiji cha Kivalali kata ya Ifunda baada ya gari lake  kupata pacha  wakati wa zikara hiyo hivyo kulazimika kutafuta baiskeli ili kufika haraka mkutanoni kusikiliza kero za  wananchi wake ,amini ni mbunge wa kwanza mkoa wa Iringa kutumia usafiri kama huu kuwafikia wananchi wake,picha nyingine akisalimianana  wananchi wa kijiji Kivalali (picha na Francis Godwin Blog)





Na Francis Godwin, Iringa
MBUNGE  wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa amevunja rekodi ya  wabunge wa jimbo hilo na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuachana na matumizi ya magari ya kifahari na kuamua kutumia usafiri wa Baiskeli kuwatembelea  wapiga kura  wake.

Huku wananchi wa kata ya Ifunda na Mgama wakisema kuwa ubunge wa Mgimwa si wa mwaka mmoja ama mitano bali  hadi mwaka 2025 hadi mwenyewe atakavyo sema yatosha . 
Mbunge Mgimwa atumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura ,wao wasema hawahitaji mbunge mwingine hadi 2025

Mbunge huyo alifikia hatua hiyo  jana  baada ya mmoja kati ya magari yake mawilio yaliyokuwa katika msafara wake kukwama kulazimika kutumia usafiri huo  wakati wa ziara yake ya siku mbili ya  kuwatembelea  wapiga kura  wake na kupokea changamoto mbali mbali

Alisema  kuwa amelazuimika  kuumia usafii huo  ili kuwafikia wananchi wake kwa wakati kutokana na gari lake kupata tatizo japo aliasema usafiri huo ni  wa kawaida kwani  amekuwa akiutuimia toka utoto wake na  kuwa kazi ya ubunge si kujitenga na wananchi bali kuwa karibu nao kwa mazingira ambayo wao  wamekuwa wakiishi .

Mgimwa  alisema  kuwa katika ubunge wakle kamwe hatajitenga na  wananchi wake na badala yake ataendelea kuwa karibu nao kwa kuishi kama  wao wanavyo ishi ili kujua changamoto zao badala ya  kutumia usafiri wa magari kila  wakati .

Alisema  kuwa si kawaida kwqa mbunge kutumia usafiri huo wa Baiskeli ila kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi ni lazima kuwa tayari kutumia usafiri wowote kulingana na mazingira na  kuwa kamwe wana Kalenga wasitegemee kuwa walikosea kumpa ubunge ila wanapaswa kuendelea kujivunia kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwani ni nafasi ambayo anaipenda na kamwe hatawaangusha katika  kuwatumikia .

Japo aliwataka  wana kalenga  kuepumka kubadili wabunge kama nguo zao kwani kufanya hivyo ni kujirudisha nyuma katika maendeleo na kuwataka kujifunza  kutoka katika majimbo ambayo wabnunge  wake wameongoza kwa zaidi ya vipindi vitatu na maendeleo yameonekana .

Pia alisema  kuwa huu si wakati wa wana kalenga kuwakumbatia wale  ambao wanajipitisha kutaka kuungwa mkono mwaka 2015 na  badala yake  wanapaswa kuwachukia watu hao na kuwaogopa kama ugonjwa wa ukoma kwani fedha  wanazotoa kwa sasa ni fedha ambazo  wanawakopesha kwa riba kuibwa ya  kutaka ubunge ili kurudisha fedha hizo na sio kuwatumikia wananchi.
Mwisho


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...