Wananchi wakitazama mwili wa Marehemu kwenye eneo la tukio |
Kwa mujibu wa tovuti ya farajimfinanga.com Mmoja wa mashuhuda Kapambara Juma amesema kwamba, chanzo cha ajali hiyo ambayo imetokea jana jioni ni mwendokasi wa Roli hilo Aina ya Fuso lenye no.T 161 AQR Mali ya Ndeleye Trans lilokuwa linaendeshwa kwenye barabra ya Lami iendayo nchi za Rwanda na Burundi.
wananchi wakiwa wemezunguka eneo la ajali baada ya mwili wa Marehemu kuondolewa na polisi. |
Tukio
hilo limetokea mwezi mmoja tangu ajali nyingine iliyomuua msichana
ambaye hakujulikana, hali iliyosababibisha Jeshi la Polisi kitengo cha
usalama barabarani wilayani humo kuahidi kuyaondoa mara moja magari
makubwa yanayoegeshwa na kubana njia barabarani hapo.
Wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo wamehoji ahadi ya Jeshi la Polisi kuyaondoa magari hayo huku yakizidi kuongezeka kila siku na wala hakuna hatua zozote za utekelezaji zilizoweza kuchukuliwa.
Ofisa wa kikosi cha usalama barabarani aliyefika kwenye tukio hilo Thoma Muyonga alipotakiwa kuzungumzia malalamiko hayo amesema, Polisi kwa kushirikiana na serikali walikuwa wakikamilisha hatua za kuhamisha maegesho hayo kuyapeleka nyakato hatua ambayo imekwisha kamilika.
Jeshi la Polisi wilayani humo linamtafuta dereva wa lori hilo ambaye alikimbia baada ya kupata ajali ambapo mazishi ya mwili wa Marehemu Mohamed yamefanyika jioni katika makaburi ya waislamu yaliyopo mtaa wa majengo mjini kahama.

Baiskeli aliyokuwa akiendesha Marehemu. |
Gari linalodaiwa kumgonga Marehemu. |