Mtangazaji wa 93.7 E-FM kupitia kipindi cha Genge, DVJ Penny ambaye wiki kadhaa zilizopita picha zake zilisambaa mtandaoni zikimuonyesha akiwa amevishwa pete ya uchumba huku mwanaume aliyefanya tukio hilo akiwa ni kitendawili, hatimaye mwanadada huyo ameibuka na kumuweka wazi mpenzi wake…..
Akiongea na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa Penny amesema kuwa jamaa aliyemvalisha pete ni kigogo mwenye pesa chafu anayemiliki migodi kadhaa ya madini anayefahamika kwa Jina la Johnson raia wa Angola….
Akiongea kwa kirefu zaidi, msichana huyo alisema,” Watu wanaumiza vichwa vyao kufikiri ni nani aliyechukua maamuzi magumu ya kumvisha pete Penniel, lakini ukweli ni kwamba huyo jamaa ni mtu mwenye pesa chafu raia wa Angola,”
Rafiki huyo amesema kuwa kutokana na jeuri ya pesa ya kigogo huyo, Penny anatarajia kufanyiwa bonge la harusi na watafanya kila namna ili Diamond awe mtumbuizaji katika sherehe hiyo….
“Huko kwao Johnson anamiliki migodi zaidi ya kumi ya Almasi na yupo hapa nchini kwa ajili ya uwekezaji, anampenda sana Penny na ameahidi kumfanyia kila atakacho,” alisema msichana huyo.
Baada ya kupata umbea huo, Mwandishi alimtafuta Penny kupitia simu yake ya mkononi na kumhoji juu ya taarifa hizo ambapo alikiri kuwa na mchumba na kusema ndoa iko karibuni.
Alipoulizwa kuhusu Diamond kutumbuiza kwenye harusi yake, Penny alijibu;
“Kutakuwa
na wasanii wengu tu sasa na yeye kama atapokea mwaliko wa
kuja kutubuiza atapatiwa nafasi, akiona vipi, halazimishwi.”