Assah Mwambene
Na Mwandishi Wetu
Siku chache baada ya
Serikali kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yaliyokuwa yakitoka kila
siku, jana imetoa tamko lingine kwa uongozi wa kampuni hizo.Msemaji wa Serikali
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Assah Mwambene,
ameitaka Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kuacha mara moja
kuchapisha gazeti hilo
katika mtandao.
Alisema Serikali
imelifungia gazeti hilo
kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia Septemba 27, mwaka huu, lakini limeendelea
kuchapishwa kwenye mtandao wa intaneti kinyume cha amri iliyotolewa."Kufanya hivyo
ni kosa,...Serikali tumewaandikia barua ya kuwataka waache kufanya hivyo mara
moja, Serikali italazimika kuchukua hatua kali zaidi kama
amri hii itapuuzwa," alisema.
Bw. Mwambene pia
aliitaka Kampuni ya New Habari 2006, ambayo inamiliki gazeti la Mtanzania
ambalo limefungiwa kwa kipindi cha miezi mitatu, kuacha kuchapisha gazeti la
Rai kila siku ambalo awali lilikuwa likitoka kwa wiki.
Alisema Gazeti la
Mtanzania lilifungiwa Septemba 27 mwaka huu, ambapo hivi sasa kampuni hiyo
inachapisha Gazeti la Rai kila siku badala ya wiki bila kibali cha Msajili wa
Magazeti."Hilo nalo ni kosa, Serikali inawataka kuacha mara moja
kuchapisha gazeti hilo kila siku na warudie
ratiba yao ya
kuchapisha mara moja kwa wiki hadi maamuzi mengine yatakapofanyika,"
alisema.
Aliongeza kuwa, Serikali imeyafungia magazeti hayo kwa kuzingatia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 1977 hivyo hawakukurupuka kuchukua uamuzi huo.Alisema uamuzi huo ulitolewa baada ya kufuata taratibu zote za msingi pamoja na kuwasikiliza wahusika