Hivyo Kamati Kuu imeamua kuwavua Uanachama ndugu Samsoni Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo kuanzia tarehe ya jana baada ya maamuzi ya kikao cha Kamati
Kuu. Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya. Dr. Slaa anasema malengo ya waraka wa mabadiliko hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa Viongozi wa Chama. Mwisho Chama kinawatangazia Wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na Washirika
wake kwa jina la Chama.