Live Updates: Press Conference - Leo Tarehe 05/01/2014 Makao Makuu ya CHADEMA

M/Kiti wa Chama Taifa ndio ameingia maeneo haya ya Ofisini akitokea Viwanja vya Karimjee muda wowote kuanzia hivi sasa Mkutano huu na Waandishi wa Habari
utaanza rasmi ndugu Wananchi. Ikumbukwe kuwa M/Kiti wa Chama Taifa ndie ambae amekuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara zote juu ya Maazimio ya Kamati Kuu baada ya Vikao
hivyo. M/Kiti Taifa ndie Msemaji Mkuu wa Chama. M/Kiti Taifa ameingia ofisini kwa Katibu Mkuu na muda wowote kuanzia hivi sasa M/Kiti atakuja kuzungumza na Waandishi wa Habari akiambatana na Ujumbe wa
Wakurugenzi na Maofisa wa Chama. Viongozi Wakuu akiwemo Katibu Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wameshawasili hapa na
sasa Mh. John Mnyika ndio anawakaribisha Waandishi wa Habari na Kutoa salamu za utangulizi Mnyika anaanza kwa kuomba radhi kwa press kuchelewa anasema ni kwasababu ya uzito wa hoja zenyewe kwasababu Kamati Kuu iliiagiza Sekretarieti kuandaa
tamko la leo. Pia Mnyika amewatambulisha Viongozi wa Kanda waliopo mahali. M/Kiti hayupo hapa mbele na badala yake Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa ndie
anazungumza na Waandishi wa Habari na tayari ameshaanza kuzungumza

Katibu Mkuu nae anaanza kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kuanza press akiungana na John Mnyika pia Katibu Mkuu anasema kuwa atasoma neno kwa neno
kutokana na umuhimu wa hoja yenyewe! Ameanza kusoma na kusema kamati kuu ilikuwa ni ya dharura iliyokuwa na lengo la kuwajadili Wanachama watatu Dr. Kitila
Mkumbo, Zitto Kabwe na Samsoni Mwigamba. Dr Slaa anaonyesha kabrasha lenye nyaraka mbalimbali ikiwemo mkakati wa mabadiliko 2013, mashtka ya watuhumiwa na nyaraka nyingine muhimu. Sasa Dr. Slaa
anasoma mashtaka yote 11 ya Watuhumiwa kama walivyokabidhiwa kwa maandishi

Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila
Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake. Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema
yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...