Ray C.
Ray C alifunguka hayo kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa
Instagram hivi karibuni ambapo bila hiyana alishindwa kuzuia hisia zake
kama binadamu, akasema anatamani sana kupata mume anayempenda ili azae
naye watoto wawili.Ray C ambaye hivi sasa yupo mstari wa mbele katika harakati za kupiga vita madawa ya kulevya, alisema anatamani kuwa na mume kwa sababu hataki familia ya mzazi mmoja kulea watoto kama alivyolelewa yeye na mama pekee.
“Mimi nimelelewa na mama tu, malezi hayo siyo mazuri kabisa. Sipendi yatokee kwa wanangu ndiyo maana natamani nimpate mtu ambaye ananipenda kutoka moyoni, tufunge ndoa kabla ya kuzaa,” alisema Ray C.
Baada ya mwanamuziki huyo kuandika ujumbe huo mtandaoni, walijitokeza wadau wengi ambao walikuwa wakimtakia baraka ili ndoto zake zikamilike huku wengine wakijitokeza na kumwambia wako tayari kumuoa.