Pichani
ni Uongozi wa juu wa Chama cha Wasanii wa Filamu hapa nchini.a.k.a
Bongo Muvi,kulia ni Katibu Mkuu,William Mtitu,Mwenyekiti,Steven Mengere
a.k.a Steve Nyerere,Katibu Msaidizi Bi.Devotha Mbaga,Mweka hazina Mkuu,
Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti ,Mahsein Awadh maarufu kama
Dk Cheni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa hapo
jana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo waliokutana kwenye viwanja vya Lidaz club,jijini Dar.
Pichani
ni Mwenyekiti wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi,
Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika
wadhifa huo wa Uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka
kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia
yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa
filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii
wake wananufaika na kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa
ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na
Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa.
Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania
haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika
kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu.
Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond
peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu,Dk Cheni akiwashukuru wadau
mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine
kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa
ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama
hicho
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi,William Mtitu
akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika
suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao
watahakikisha chama chao kinasimama imara.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo
Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa
tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao
wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha
inaendelea kukua siku hadi siku.
Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere.