Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex Energy Bw
Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali
(hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa teknolojia
mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza Umeme,mkutano huo
umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo
mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani mbele kushoto ni
Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Medard Rweikiza pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Francis Kibhisa wakiwaonesha na
kuwaeleza baadhi ya Waandishi wa Habari namna moja ya kifaa cha kisasa
kabisa chenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Mwanga wa Jua
(Solar).
Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Rex Energy,Bwa.Francis Kibhisa akitoa ufafanuzi wa namna moja
ya kifaa (pichani),kinachotumia teknolojia ya kisasa katika suala zima
la kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua (Solar Power) mbele ya
Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Bwa.Francis alibainisha kuwa kifaa
hicho kina uwezo wa kuwasha vifaa vya ndani kama vile taa,redio, friji,
TV kwa wakati mmoja,na huuzwa kwa gharama nafuu.Pichani kulia ni Ofisa
Mauzo wa kampuni ya Rex Enegy,Bwa.Medard Rweikiza akisikiliza
Baadhi ya Wafanyakazi wa
Kampuni ya Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kumaliza
mkutano wao na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi.