Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye
kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko
la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido
Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia
mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara
wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili
ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa
zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali
mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi
soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni
John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva
wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya
soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa
mpira wa sokoni Sido.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira
kumalizika.