Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto)
akikabidhi nakala za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la
Wahariri Neville Meena (katikati) wakati wa mkutano baina ya Tume hiyo
na Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee
Jijini Dar esa Salaam leo Alhamisi Januari 2, 2014. Anayeshuhudia ni
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi
Mukajanga.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (wa pili kulia)
akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa mkutano
baina yake ya Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi
wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 2. 2014. Wengine
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi
Mukajanga, Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Makamu Mwenyekiti wa Tume,
Jaji Mkuu mstaafu Augstino Ramadhani.
(PICHA NA TUME YA KATIBA).