TASWIRA KUTOKA MAHAKAMA KUU WAKATI WA KUSIKILIZWA PINGAMIZI LA ZITTO KABWE

 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Dar es Salaam, SACP Marietha Minangi, wakati akiwasili Viwanja vya Mahakama Kuu.
Mmoja wa kijana aliyekamatwa na askari baada ya kuleta fujo eneo la mahakama.
Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo wananchi eneo la Mahakama Kuu.
Wafuasi wa Zitto Kabwe.
Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwahutubia wananchi waliofika mahakamani hapo baada ya hukumu ya Zitto kuahirishwa mpaka kesho saa nane mchana..
Wanausalama wakipanga mikakati ya kuimarisha ulinzi eneo la Mahakama Kuu jijini Dar.
Polisi wenye mbwa wakipita eneo la mahakama kuimarisha ulinzi.
Mmoja wa wafuasi wa Zitto akiwa na bendera.
Mwanasheria wa Zitto Kabwe, Albert Msando (kushoto) akitoka mahakamani baada ya hukumu kuahirishwa.
Wanahabari wakitoka eneo la mahakama.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa au kutotoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutojadili uanachama wa Zitto Kabwe mpaka kesho saa nane mchana!
(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...