Upinzani
nchini Afrika Kusini unataka uchunguzi kufanywa kuhusiana na madai ya
ubadhirifu wa pesa zilizotengwa na chama hicho kwa matumizi wakati wa
hafla ya mazishi ya hayati Nelson Mandela.
Matakwa
hayo ya upinzani yametolewa baada ya taarifa za jarida moja kusema kuwa,
sehemu ya dola elfu miatano zilizotengwa mahsusi kwa shughuli ya
kuwasafirisha waombolezaji katika mazishi ya Mandela, zilitumiwa kwa
shughuli nyinginezo ikiwemo kushonesha fulana za chama cha ANC
Duru
kutoka mji wa East London zimesema takriban dola laki tano zilitengwa
kando kusaidia katika kuwasafirisha waombolezaji wakati wa ibada maalum
ya Nelson Mandela.Chama cha ANC ambacho kimezongwa na kashfa za ufisadi
hakijajibu tuhuma hizo.
Hata hivyo fedha hizo zilielekewa kwa kampuni nyingine ambazo hazikua zikitoa huduma za uchukuzi.
Diwani mmoja wa chama cha Democratic Alliance ameambia BBC kwamba zilitolewa risiti bandia.
Manispa
hio imesema inasubiri ripoti kamili kuwasilishwa mbele yake mwishoni mwa
mwezi huu. Utawala wa Rais Jacob Zuma unakabiliwa na uchaguzi mgumu
mwaka huu wakati ukikumbwa na sakata nyingi za ufisadi