MAN WALTER AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA NYIMBO ALIZOMTENGENEZEA LADY JAYDEE, SOMA HAPA KUJUA

Producer wa Combination Sounds, Man Walter amesema kufanya kazi na Lady Jaydee aliyemtayarishia hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya ni kitu kilichomsogeza mbele katika career yake.clip_image001“Kufanya kazi na msanii mkongwe na ukazidi kumsogeza pale ambapo alifikiria kufika inakuwa ni faraja sana kwa maana na mimi nimeongeza kujiamini kwamba naweza pia kufanya maajabu zaidi, sababu mwanzoni ilikuwa ni ndoto kufanya kazi na Jaydee, nilikuwa napenda. Nashukuru nimefanya na nimefanya vizuri,” Man Walter aliyetajwa mwaka huu kuwania tuzo ya Mtayarishaji Bora wa muziki wa kizazi kipya ameiambia Bongo5. “Hata kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Music Awards kunanifanya nijifariji na ni ngoma ambazo ninazitegemea sana.”
Walter amesema bado anaendelea kufanya kazi zingine na Lady Jaydee. Projects zake nyingi ni kama amezihamishia Kombinenga. Nashukuru sana kwa hilo kwasababu ametokea kuniamini sana mpaka kunipa kazi nyingi ambazo nitazifanya,” amesema.
Producer huyo amesema kazi za wasanii wengine zitakazotoka kwenye studio yake ni pamoja na ile ya Christian Bella aliyomshirikisha Ommy Dimpoz. Wimbo huo amesema ni maalum kwa wanawake na unatarajiwa kutoka hivi karibuni huku akidai kuwa ni lazima utafanya vizuri.
>>BONGO5


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...