| Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao | 
| Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha umadhubuti wa bori lake | 
| Mwanahabari huyu Oliva Motto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha | 
| Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubinifu huo | 
Na Francis Godwin, Iringa
Amini
 usiamin. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 
BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine. Linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, mkoani Iringa Bw.Kenny Mwangoka.
Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya 
kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika 
vibaya. Jitihada zake za kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya 
hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.
"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha 
bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema, na kuongeza kuwa baada 
ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali
 anazopita nalo.
"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na 
maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni 
pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema, na kuongeza 
kuwa  atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane mwaka huu kama moja ya 
njia za kuhamasisha upandaji wa miti. 
 

