UINGEREZA YAJIVUNIA KUWA NCHI INAYOONGOZA KATIKA UWEKEZAJI NCHINI TANZANIA

???????????????????????????????????????????????Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi mpango wa bima ya afya na maafa wa WESTADI wa mfuko wa Jamii wa NSSF jijini London, akiwa na Mkurugenzi wa NSSF Dkt RAmadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo Bw. Abubakar Rajabu (kushoto) . Mwenye miwani kati ni Bw. Aboubakar Faraji aliyekuwa mwongoza sherehe wa siku hiyo ambapo Dkt Kikwete alikutana na kuzungumza na Watanzania waishio Uingereza.
AK385518Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Bw. Hague alipomtembelea ofisini kwake jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014AK385520Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014bk2Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Duke of York ambaye pia ni  Balozi wa Biashara wa Serikali ya Uingereza  HRH Prince Andrew katika kasri ya Malkia ya Uingereza ya Buckingham Palace jijini London Machi 31, 2014
bk8Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014bk10Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Jiji la London Mstahiki Alderman Fiona Woolf alipomtembelea ofisini kwake Mansion House jijini London Machi 31, 201bk12Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyabishara wakubwa na wawekezaji wa Uingereza aliokutana nao katika mkutano wa biashara na uwekezaji katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola jijini London Machi 31, 2014bk21Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wadau mbalimbali wa biashara na uchumi  wa Uingereza aliokutana nao katika ukumbi wa  Chatham House  jijini London Machi 31, 2014
PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………
Uingereza inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 10 Downing Street,  Leo tarehe 31 March, 14, ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
“Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania”
 Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
Rais Kikwete amewasili nchini Uingereza tarehe 30 Machi, 2014 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku 3 kufuatia mualiko wa Bw. Cameroon ambaye pia amemuomba Rais Kikwete aendelee kutoa mchango wake wa mawazo katika masuala ya kimataifa hasa baada ya mwisho wa muda wa malengo ya millennium ya 2015.
Tunakaribia mwisho wa muda wa malengo ya millennia Mwaka 2015, tutahitaji kuweka vipaumbele vingine baada ya hivyo kama kuondosha umaskini, Maji safi na salama, masuala ya ufisadi na utawala bora, natumaini utaendelea kutoa mchango wako baada ya malengo hayo kufikia tamati” Waziri Mkuu Cameron amemuambia Rais Kikwete ambapo Rais amekubali ombi hilo na kuahidi ushirikiano wake.
Mapema leo asubuhi Rais amekutana na mtoto wa Mfalme Prince Andrew katika makazi ya Malkia ya Buckingham ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali ya Kimataifa na Kijamii.
Kabla ya kwenda Buckingham Rais amefungua mkutano kuhusu uwekezaji na kuelezea fursa na nafasi zilizopo za uwekezaji nchini Tanzania na kuelezea kwanini wawekezaji watakuwa wanafanya uamuzi bora kwa kuwekeza Tanzania kuwa ni pamoja na;

“Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana”
 amesema.
Katika ziara yake Rais pia amekutana na Mstahiki Meya  wa Jiji la London Mama Alderman Fiona Woolf na kukaribishwa rasmi Jijini London. Mstahiki Meya  anatarajia kutembelea Tanzania, Mwezi Septemba Mwaka huu.
Rais alipowasili London tarehe 30 Machi,2014, alikutana na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na kuwaeleza maendeleo yaliyopo nchini Tanzania.
Rais anaendelea na ziara yake nchini Uingereza
Mwisho.
Imetolewa na;
Premi Kibanga.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
London Uingereza
31 Machi, 14


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...