Wasanii
hao wanazishutumu tuzo hizo kwa kutozitendea haki nchini za Afrika
Mashariki mwaka huu na kwa kuwapendelea wasanii wa Afrika Kusini na
Nigeria zaidi. “Uganda imeumia zaidi kwasababu kutajwa kwao pekee ni kwa
collabo na Amani,” msanii mkubwa wa Kenya ambaye hakutaka kutajwa jina
lake aliuambia mtandao huo.
Umeandika
kuwa wasanii waliotarajiwa kutajwa kwenye tuzo hizo ni AY, Ommy Dimpoz
na Lady Jaydee, Tanzania, P-Unit, STL, Elani na Wyre wa Kenya na Jose
Chameleone na Navio wa Uganda. Mtandao huo umeripoti kuwa wasanii wengi
zaidi wanapanga kutoshiriki kwenye show za utangulizi za Road to Mamas
zitakazofanyika Dar es Salaam kwa Afrika Mashariki.