VIFO VYA MASTAA VYAMPA HOFU SUPERSTAAR DAVINA

http://api.ning.com/files/LAl787uzrCCfK3zrV0j*I6DTX3VQYjeVRgjFvkx8-62CGf6b-hS92eScXQ538lO5y7oDmZwPn2K8GwIb6HMnlMWNF5ZuLN6q/davina.jpg
Stori: Hamida Hassan
HOFU! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amewashauri wasanii kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwani anaona jinsi wasanii wanavyozidi kupukutika.
Halima Yahya ‘Davina’.

Kuonesha msisitizo, Davina amewasihi wasanii wenzake kuacha kutumia pombe na kwa wale ambao wanatajwa katika ishu za usagaji, waache mara moja kwani Mungu anajidhirisha kila kukicha kwamba yupo na watu waishi kwa matakwa yake.
“Nawashauri wenzangu kuwa usanii siyo ufuska kama baadhi wanavyofanya, tumrudie Mungu na tujifunze kupitia vifo vya mastaa wenzetu, kufa kupo tu lakini je, tumejiandaa vipi?” Alihoji Davina kwa hofu.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...