Baada ya Elizabeth Michael kukana kushirikishwa na kundi la mapacha
kwenye wimbo wao mpya ‘Time For The Money’. Kundi la Mapacha limeeleza
jinsi lilivyoipokea taarifa hiyo.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Kulwa wa Mapacha amesema kitendo
alichokifanya Lulu ni dharau kubwa kwao na kwamba inawezekana ameona
hataki kusikika kwenye wimbo waliofanya wao.
“Sisi tuliamua kumtaja kwa respect kwa kuwa tulipenda alichofanya
kwenye ile beat ambayo sisi tuliamua kuiimbia kwa kutumia chorus yake.
Lakini yeye ameamua kutu-disrespect. Sasa sisi tumeamua hata kama wimbo
huo ukipata tuzo basi yeye hatutamtaja...ametudharau.”Alisema Kulwa.
Aliongeza kuwa hivi sasa wameamua kulifuta jina la Lulu na kwamba hata wimbo huo utakapokuwa unapigwa asitajwe kabisa.
“Sasa hivi tunasimama kama Magenge peke yetu. Tumeachana na masuala ya Lulu, hatutamtaja
na tunafuta jina lake kabisa sasa hivi tunabaki Magenge tu.”
Tulipomuuliza kwa nini hawakuwasiliana nae awali angalau kumshukuru
kwa chorus aliyowafanyia ili wapate mrejesho mapema. Alisema wao
hawajawahi kuonana nae wala kuwasiliana nae hata siku moja.
“Tungewasiliana nae vipi, si unajua hawa watoto unaweza kuwapigia
simu wakaacha hata kupokea..si unajua mwanangu. Sisi tungempata wapi
sasa. Tud yeye alituambia ni Lulu na sauti yake kweli ni yeye. Sasa kama
anakataa bana tunaachana nae."
Baada ya Mapacha kutambulisha wimbo wao na taarifa kumfikia Lulu leo, aliandika kwenye Instagram kwa mshangao mkubwa.
“Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's voice'
I swear sina idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!????
Dah...hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.”