Kabla ya kujadiliwa kwa bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii
ilianza sehemu ya maswali na majibu kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa
nne.
Naibu
waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia ndio alijibu swali la
Catherine Magige kuhusiana na udhalilishaji wa Wanawake unaofanywa
kwenye kumbi mbalimbali za starehe Tanzania.
Waziri
Nkamia alisema ‘nakubalia kabisa kwamba kumbi za starehe zimekua
zikitoa burudani na ajira kwa vijana hapa nchini lakini ndani ya kumbi
hizo kumekua na vitendo vinavyofanyika kinyume na maadili ikiwemo
udhalilishaji wa Wanawake’
Katika
kukomesha hali hiyo serikali kupitia baraza la sanaa BASATA wamefanya
vikao kadhaa na wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni, wakuu wa polisi,
wamiliki wa kumbi na wanaojihusisha na uchezeshaji wa mtindo wa kanga
moja ili kujadili ukiukwaji wa maadili kwenye sanaa
Waziri amesema
Pia
serikali imeacha kutoa usajili kwa vikundi kama cha kanga moko kwa kuwa
uchezaji wake unakwenda kinyume na maadili ya Tanzania na kutoa onyo
kwa wamiliki wa kumbi, Wasanii na hata asasi zinazojihusisha na sanaa
ambazo hazifati maadili
Amesema
Wasanii
waliopewa Onyo ni Ney wa Mitego, Shilole, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na
kwa upande wa kumbi ni Mama’s and Papa’s lakini pia maonyesho ya urembo
ya Miss Utalii yalifungiwa ambapo pia Serikali imeunda kamati ya kitaifa
ya kuzuia ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake/Wasichana watoto